TOC

This article is currently in the process of being translated into Kiswahili (~99% done).

Introduction to HTML:

What is HTML?

HTML ni nini?

HTML ni lugha ya markup inayotumika kueleza tovuti katika hali yake ya msingi kabisa. Ni lugha kuu ya markup ya kurasa za tovuti. HTML ni ufupisho wa Hyper Text Markup Language. Wakati kivinjari cha tovuti kama vile Internet Explorer, Firefox au Chrome inaonyesha kurasa la tovuti, kile ambacho hufanyika ni kwamba kivinjari kinakisoma nakala ya HTML. Nakala yenyewe yaweza kuwa na mistari 10 au hata mia za mistari, kivinjari haijali urefu wa mistari katika nakala - kile kivinjari kitafanya tu ni kukisoma hiyo nakala.

Na hii ni nia kuu ya HTML - kuifanya maudhui ya nakala ya HTML kupatikana na kivinjari. Kando na kuifanya nakala yako kupatikana na kivinjari cha tovuti, HTML pia huongeza semantiki kwenye maudhui hiyo - hii ina maana kuwa kivinjari cha tovuti na injini cha kutafuta hujua ni aina gani ya maudhui umeweka kwenye nakala yako na hivyo kutambua jinsi ya kuishughulikia.

Kimsingi, nia ya HTML ni kuongeza maana kwenye kurasa za tovuti (Wengine wanaamini kuwa HTML inapaswa kuathiri sura ya kurasa ya tovuti, lakini hilo kwa sana ni swali la dini na tutaliangazia baadae) ili kivinjari iweze kuionyesha.

HTML5 ni nini?

Kwa hivyo ni nini tofauti kati ya HTML na HTML5? Tutaliangalia hili swali kote kwenye mafunzo, lakini kitu moja ambacho ni muhimu kukizingatia ni kuwa chochote ambacho unawezakuwa umejifunza kuhusu HTML bado ni halali ikija kwa HTML5 - haina haja kutupa chochote kando.

HTML5 ina shirikisha vipengele vingi vipya na tutaviangalia vipengele hivyo kibinafsi tunapoendelea. Lakini kwa kweli, HTML5 sio tu toleo la tano la HTML - HTML5 kiasili kiliumbwa na kikundi cha watu ambao hawakua wanahusika kirasmi na sifa za HTML. Kuielewa maeneo ya HTML sio kazi rahisi - shida kuu ni kuwa, watu wengi hukitumia neno HTML5 wakati ambapo kile wanachokiashiria ni "HTML5 na kila kihusisho chake na sifa zingine kama vile CSS3".

Katika mafunzo haya cha kuangaziwa kitakuwa ni vipengele vya ndani vya HTML5 na jinsi ya kuvitumia na jinsi intofautiana na HTML 4 "nzee".

Unapoitumia HTML5, unapaswa kujua kwamba sio vipengele vyote vipya vinaweza kutumika na vivinjari vyote. Vivinjari tofauti huwezesha vipengele tofauti tofauti kutumika kwa hivyo itakubidi kufanya hila hapa na pale kuzifanya vipengele hivyo vya HTML5 kufanya kazi kwa usahihi.

Lakini jambo moja ni la hakika - HTML5 ni hatima, hivi ndivyo kurasa za tovuti vitakua vikitengenezwa, Apple na Google wanawezesha vipengele vya HTML5 kwa kiwango kikubwa. World Wide Web washawacha kazi yao ya kizazi kijacho cha xHTML ili kukiunga mkono HTML5, sasa acha tuanze!


This article has been fully translated into the following languages: Is your preferred language not on the list? Click here to help us translate this article into your language!
adplus-dvertising